Friday, 27 January 2017
Angalia Data za World Bank; Nani Zaidi - Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Magufuli Kwa Uchumi Tanzania
Labda hiyo grapgh haoinekani vizuri, lakini inachoonyesha ni kwamba kulingana na data za Benki ya dunia, tukitumia GDP per capital growth rate, katika kipindi cha Mwinyi, Mkapa na JK, Mkapa ndio aling'ara kwenye kuinua ukuzi wa uchumi, tunapolinganisha alipoingia na alipotoka, na kwa ujumla.
Japo kwa Mwinyi tunachoona ni miaka yake mitano ya mwisho - inaonyesha aliuacha uchumi katika hali mbaya kuliko kipindi chake cha kwanza cha miaka mitano. Mwinyi peke yake aliingiza Tanzania kwenye negative GDP per capital growth rate, hadi wastani wa -3%.
Mkapa alipochukua nchi aliuboresha uchumi zaidi sana ya Mwinyi alipouacha. Kuelekea mwishoni mwa kipindi cha Mkapa kasi ya ukuzi ilipungua, labda ni kipindi kila mtu alianza kuchukua chake! Kwa ujumla ukuzi wa uchumi wakati wa Mkapa ulikuwa na msimamo mzuri unaoeleweka, sio panda shuka ya Mwinyi na Kikwete.
Kikwete alipochukua toka kwa Mkapa ghafla uchumi alianza kuporoka chini zaidi ya pale alipouacha Mkapa. Jambo lililo wazi ni kwamba wakati wa Kikwete ukuzi wa uchumi ulikuwa hauna msimamo kamili, kila mwaka kupanda na kushuka kuonyesha Kikwete hakuwa na mwelekeo unaoeleweka katika mambo ya uchumi ukilinganisha na Mkapa. Kwa wastani Kikwete aliushusha uchumi kuliko alipouacha Mkapa.
Katika kipindi cha mwaka mmoja cha JPM, japo watu wanalalamika kwamba shilingi imeota miguu, lakini yeye amefikia rekodi ya GDP per capita growth rate ambayo haijawahi kufikiwa na maraisi wote waliomtangulia. Magufuli alipochukua tu nchi toka kwa Kiwete tulianza kupanda. Sasa hii inamaanisha nini kuelekea mbele tunasubiri kuona, na mwishoni mwa 2017 tutapata picha kamili.
Ila picha ya ujumla ni kwamba tangu 1990 hadi 2016 tumeenda vizuri sana. Katika kipindi cha Mwinyi na Kikwete kwa wastani hatukwenda mbele wala kurudi nyuma. Hadi sasa ni Mkapa peke yake aliyetuinua tangu mwaka 1990. Na Magufuli anaonekana ana mwelekeo wa kutuinua toka pale alipotuacha Mkapa.
NB. Data za 2016 kipindi cha JPM hapo juu ni halisi, isipokuwa zimefanywa wastani wa quarter tatu (January - September), Q1, Q2, Q3, badala ya nne za miaka mingine.
Source: GDP per capita growth (annual %) | Data
GHARAMA ZA UNGA
Wewe kama mjasiriamali au mfanya biashara unatumiaje fursa ya kupanda kwa gharama za biashara mbalimbali kuanzisha biashara yako??
Tuachie maoni yako tafadhari..
au wasiliana nasi kwa ushauri zaidi 0766865041

Hali mbaya: Makampuni ya simu yaanza kupunguza wafanyakazi. ITV yasogeza mishahara mbele
Hali tumbua majipu na kuzuia pesa za ovyo yazidi kuumiza vichwa watu hadi makampuni makubwa ya simu..
UTARATIBU WA WAJASIRIAMALI WADOGO NA WA KATI (SMEs) KUWEZESHWA KUPATA ALAMA YA UBORA YA ‘TBS’
kumbuka kuwasiliana nasi kwa ushauri zaidi 0766865041
1.0 UTANGULIZI
Serikali hutenga fedha kila mwaka kwa ajili ya kuhudumia wajasiriamali wadogo na wa kati pale wanapoomba bidhaa zao wanazozizalisha wenyewe zithibitishwe ubora. Katika utaratibu huu, wapo wajasiriamali ambao husamehewa kulipa ada yoyote kwa sababu ya mitaji yao kuwa midogo.
Ili kupata msamaha huu, vigezo vifuatavyo huzingatiwa:
Mjasiriamali hutakiwa kuwa na barua ya utambulisho kutoka ofisi ya SIDO iliyo karibu. Ni vema kuhakikisha kuwa barua inafafanua vizuri na kwa kina shughuli zinazofanywa.
Kwa wale wanaozalisha vyakula huhitajika kuwa na taarifa fupi kutoka Idara ya Afya iliyo karibu na mahali pa uzalishaji au cheti cha TFDA.
Mjasiriamali hupaswa kuwa na leseni ya biashara.
Wajasiriamali waliokwishapata leseni ya kutumia alama ya ubora hupaswa kutunza rekodi za uzalishaji na mauzo ambazo watatakiwa kuzionesha kwa wakaguzi wa TBS pindi zinapohitajika.
2.0 HATUA ZA KUPATA ALAMA YA UBORA YA ‘tbs’
2.1 HATUA YA KWANZA – MAOMBI
i) Maombi ya uthibitishaji wa ubora wa bidhaa hufanywa na mwombaji kwenda kwa Mkurugenzi Mkuu wa TBS kwa maandishi.
ii) Majibu hutolewa yakielezea taratibu na gharama zote.
iii) Majibu huambatana na fomu maalum ambayo mwombaji huijaza na kuirudisha TBS ikiwa na viambatanisho vifuatavyo:
• Mtiririko wauzalishaji wa bidhaa husika;
• Mfumo wa uongozi ukionyesha kitengo cha udhibiti ubora;
• Orodha ya malighafi anazotumia na mahali zinakotoka kwa kila bidhaa;
• Ramani inayoelekeza jinsi ya kufika kiwandani kwako;
Baada ya hapo tarehe ya kufanya ukaguzi wa awali hupangwa.
2.2 HATUA YA PILI – UKAGUZI WA AWALI
• Ukaguzi wa awali hufanywa na wakaguzi wa TBS wa kati kiwanda kikiwa katika uzalishaji.
• Sampuli huchukuliwa na kupimwa ili kuona kama zinakidhi matakwa ya kiwango husika.
• Mkaguzi huandaa taarifa kuhusu hali halisi ya kiwanda na mambo yanayostahili kurekebishwa.
2.3HATUA YA TATU – UPIMAJI
• Sampuli zilizochukuliwa hupimwa katika maabara za TBS kwa kufuata kiwango husika.
• Baada ya kazi ya upimaji kumalizika, ripoti ya maabara hutolewa kwa mwombaji.
2.4 HATUA YA NNE – UTOAJI WA LESENI
• Maamuzi kuhusu kutoa au kutotoa leseni ya kutumia alama ya ubora hutegemea tu ripoti ya ukaguziwa awali wa kiwanda pamoja na ripoti ya maabara.
• Kimsingi ripoti zote mbili zinatakiwa kuonyesha kwamba mazingira ya uzalishaji kiwandani, mfumo wauzalishaji na bidhaa iliyopimwa havina matatizo.
• Ikiwa sivyo basi mzalishaji hutakiwa kufanya marekebisho na baadaye mkaguzi wa TBS hutumwa tena na kuleta sampuli nyingine.
3.0 MUDA WA LESENI (VALIDITY OF LICENCE) YA ALAMA YA UBORA YA ‘tbs’
Leseni ya kutumia alama ya ubora ya ‘tbs’ hudumu kwa mwaka mmoja na huhuishwa (renewal) baada ya kuhakikisha kwamba taratibu zilizokubalika (Scheme of Inspection and Test, SIT) zinafuatwa.

AINA ZA MUUNDO WA BIASHARA
kumbuka kuwasiliana nasi kwa ushauri zaidi 0766865041
Utangulizi
Mojawapo ya maamuzi ya mwanzoni kabisa unayohitaji kufanya kwa ajili ya biashara yako mpya ni kuchagua aina ya muundo wa biashara unaoona unakufaa. Uchaguzi unaofanya ni muhimu kwa kuwa utaathiri uwezo na mamlaka ya biashara yako kufanya au kutofanya jambo fulani. Kuwa na aina na muundo sahihi wa biashara kutakusaidia kukuongoza wakati biashara yako iko kwenye mafanikio au wakati wa taabu.
Muundo sahihi wa biashara ndio utakuongoza nini cha kufanya ikiwa utashtakiwa, na kwa namna gani wewe na biashara yako mtatozwa kodi. Kimsingi ziko namna kuu tatu za kuunda biashara, zimeelezewa hapa chini
Biashara inayoendeshwa na mtu binafsi peke yake
Biashara inayomilikiwa na kuendeshwa kwa Ubia
Kampuni yenye ukomo wa madeni
Biashara inayomilikiwa/ kuendeshwa na mtu mmoja
Biashara inayoendeshwa na mtu binafsi peke yake, au Mfanyabiashara pekee ni aina ya biashara ambayo imeenea sana miongoni mwa wajasiriamali nchini. Hii ni biashara ambayo ni rahisi sana kuanzisha kwani mmiliki hufanya usajili wa jina la biashara na kutimiza masharti mengine machache kabla ya kufungua bishara.
Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) imetoa mwongozo wa kusajili jina la biashara ambapo mjasiriamali atatakiwa kulipia wastani wa Shilingi 20,000. Mwongozo huu unapatikana kwenye tovuti ya Brela. Mada zijazo pia tutajadili namna ya kusajili biashara.
Biashara inayomilikiwa na mtu mmoja inaweza kuendeshwa kwa jina la mmiliki au jina jingine lisilo lake. Biashara ya aina hii imejipatia umaarufu mkubwa sana kutokana na urahisi wake, haswa katika uanzishaji, pamoja na gharama ndogo. Mfanyabiashara anahitaji tu kujisajili au kusajili jina lake na kupata leseni na hivi hutosha kuanza kufanya biashara.
Hasara kubwa ya kipekee ya muundo huu wa biashara ni kuwa mmiliki anabeba majukumu kwa madeni yote ya biashara yake. Hivyo ikiwa atapata matatizo ya kifedha, wadeni wanaweza kufungua kesi/ madai dhidi yake na yakifanikiwa yeye binafsi atawajibika kulipa madeni hayo kutoka kwenye vyanzo binafsi vya fedha.
Ubia
Hii ni biashara inayotambulika kisheria inayofanywa na watu wawili au zaidi wanaoshiriki katika umiliki, utendaji na faida au hasara za biashara hiyo. Ziko aina kuu mbili za ubia, ubia wa jumla (usio na ukomo wa madeni) na ubia wenye ukomo wa madeni.
Katika ubia usio na ukomo wa madeni (ubia wa jumla), wabia wanaendesha biashara na wanawajibika kwa madeni ya biashara na mali zao binafsi zinaweza kulipia madeni hayo. Kwenye ubia wenye ukomo wa madeni, baadhi ya wabia huwa na ukomo wa kuwajibika kwa madeni ya biashara na baadhi huwa hawana. Wale wasio na ukomo wa kuwajibika kwa madeni ya biashara wanamiliki biashara na wanawajibika binafsi kwa madeni ya biashara, na wale wenye ukomo huwekeza tu, hawana nguvu ya moja kwa moja katika maamuzi ya biashara na hawawajibiki kuchangia fedha binafsi kulipa madeni ya biashara.
Uwajibikaji binafsi wa wabia kwa madeni ya biashara ni suala kubwa la kufikiria iwapo unatazamia kuendesha biashara kwa mfumo wa ubia. Kama ilivyo kwa wafanyabiashara wanaomiliki biashara peke yao, wabia wanawajibika kwa fedha zao binafsi kulipia madeni ya biashara. Kila mbia wa jumla (asiye na ukomo wa madeni) anaweza kufanya maamuzi na kuingia katika makubaliano ambayo wabia wenzake wote watayaheshimu na yatawaathiri (kutegemeana na makubaliano/ mkataba wa ubia wao) kwa niaba ya biashara.
Kumbuka kuwa biashara ya ubia ina gharama kubwa zaidi kuianzisha na kuiendesha kuliko biashara ya mtu binafsi, hii inatokana na ukweli kuwa kuna taratibu mbalimbali inabidi zifuatwe kabla ya biashara kuanza. Taratibu hizo ni pamoja na kuweka makubaliano ya namna ya kuendesha biashara, mgawanyo wa mapato na mengine mengi.
Ikiwa utaamua kuendesha biashara kwa mfumo wa ubia, hakikisha kuwa umeweka kimaandishi makubaliano au mkataba kuonesha namna maamuzi yatakavyofanyika, namna ya kumaIiza tofauti zinazotokea katika kufanya maamuzi, na hata namna ya kufikia makubaliano ya kubadilisha umiliki wa biashara itakapohitajika kufanya hivyo. Makubaliano hayo yanasaidia sana pale itakapotokea kwa sababu moja au nyingine biashara imeingia katika matatizo ya kifedha au ya kiuendeshaji, au ikitokea mbia mmojawapo anataka kuondoka kwenye biashara.
Mkataba wa ubia unapaswa kukazia kuhusu kusudi la biashara na mamlaka na wajibu wa kila mbia. Ni vema kupata msaada wa kisheria kutoka kwa mwanasheria mwenye uzoefu na mambo ya biashara ndogo na za kati katika kuandika mkataba wa ubia. Mambo mengine ambayo ni muhimu yazungumziwe katika makubaliano ya ubia ni:
Umiliki utachangiwa kwa viwango gani? Si lazima viwango vya umiliki na na mgawanyo wa majukumu vilingane kati ya wabia wote. La msingi ni kuhakikisha kiwango cha kila mmoja kiko katika makubaliano.
Maamuzi yatafanyika kwa mtindo gani? Ni vema kuweka makubaliano juu ya haki za kupiga kura baina ya wabia ikiwa wameshindwa kufikia muafaka kwenye suala fulani. Ikiwa wabia ni wawili tu na umiliki wao ni nusu kwa nusu, uko uwezekano wa kushindwa kufikia muafaka katika kuamua jambo. Kuepusha hili, biashara zingine huamua kuweka mbia wa tatu, mtu anayeaminika na kummilikisha asilimia ndogo tu ya biashara, ili kusaidia kuiondoa biashara kwenye mkwamo wa aina hiyo.
Ikiwa mbia mmoja atajiondoa, kiasi cha kumlipa kitaamuliwaje? Namna mojawapo ya kuamua kuhusu hili ni kuwa na mhusika aliye nje ya ubia, mfano benki, au mhasibu kutafuta mtathmini atakayethaminisha kiasi cha kumlipa mbia anayejitoa katika ubia.
Ikiwa mbia atajitoa katika biashara, ni lini anapaswa kulipwa fedha yake? Hii inaweza kuwekwa katika makubaliano ili ijulikane bayana. Ikiwa itachukua muda mrefu, inaweza kuwa busara kuweka makubaliano kuwa ilipwe pamoja na riba. Bila makubaliano haya uendeshaji biashara unaweza kuathirika ikiwa mtu atajitoa na kiasi chote kulazimika kulipwa kwa mkupuo kwa haraka mara anapojitoa. Kampuni yenye ukomo wa madeni
Kampuni yenye ukomo wa madeni ni muundo wa shirika ambamo uwajibikaji wa wamiliki (wanahisa) kwa madeni ya biashara unakomea kwenye kiasi walichowekeza katika kampuni, au ambacho wamekubaliana kukiweka dhamana kwa ajili ya kampuni. Hivyo kampuni yenye ukomo wa madeni inaweza kuwa na ukomo kwa njia ya hisa au ukomo kwa njia ya dhamana waliyoweka wanahisa. Suala la nani anaweza kuwa mwanahisa wa kampuni binafsi linatawaliwa na sheria na kanuni za kampuni.
Kama ilivyo kwa biashara zingine zinazoendeshwa hapa nchini, Kampuni yenye ukomo wa madeni inapaswa kusajiliwa na Mamlaka ya Usajili na Leseni za Biashara, ambayo iko chini ya wizara inayohusika na Biashara. Katika usajili, hatua ya kwanza ni kupata kibali cha kutumia jina la biashara kinachotolewa na mamlaka hiyo. Nyaraka/ taarifa zifuatazo zinahitajika katika mchakato wa kuanzisha kampuni:
Jina la kampuni (ambalo lazima lipitishwe na msajili wa makampuni);
Anuani rasmi ya ofisi ya kampuni Tanzania;
Majina, anuani, na utaifa wa wanahisa wa kwanza na wakurugenzi wa kampuni (angalau wawili kwa kampuni binafsi au saba kwa kampuni ya umma).
Mkataba wa kuanzisha kampuni (unaotaja madhumuni ya kampuni) na sheria/ makubaliano yanayosimamia utendaji na maamuzi ya kampuni (inayotaja muundo wa uongozi na michakato ya maamuzi mbalimbali). Angalau nakala mbili za kila waraka zinapaswa kuwasilishwa.;
Kujaza fomu maalumu zenye tamko kuwa kampuni imezingatia matakwa ya sheria ya makampuni Tanzania; na
Kulipa tozo/ ada za kuwasilisha nyaraka, usajili, na ushuru wa stempu.
Ahsanteni..

Unataka kuanzisha biashara,jiunge nasi.....
Kwa ushauri na matangazo wasiliana nasi kwa 0766865041
Biashara yoyote huanza na wazo, ila wazo pekee halitoshi, linahitaji kufanyiwa kazi. Hapo ndipo watu wengi huweza kuanza kujisikia kuzidiwa. Si ajabu kuona mtu anakatishwa tamaa kwa kutizama msururu wa mambo yanayohitajika ili kuanzisha biashara, lakini pia kuanzisha biashara ni rahisi kuliko unavyodhani. Kama ilivyo katika lengo lolote kubwa, ukianza kwa kutengeneza malengo madogo madogo ya kutekeleza utaweza kufanya mambo yote muhimu katika kuanzisha biashara.
Jinsi ya Kuanzisha Biashara Ndogo
Kuanzisha na kuendesha biashara inahitaji msukumo, nia na kipaji. Inahitaji pia utafiti na mipango. Kama ilivyo kwenye mchezo wa drafti, mafanikio kwenye biashara ndogo huanza na maamuzi sahihi katika hatua za mwanzoni. Ikumbukwe pia hapa kuwa pamoja na kwamba makosa madogomadogo ya mwanzoni yanaweza yasiue biashara yako, inahitaji ujuzi, nidhamu, na bidii kuyasahihisha.
Ili kuboresha uwezekano wa kufanikiwa, unapaswa kutenga muda wa kujichunguza na kutathmini malengo yako kibiashara na malengo binafsi. Tumia taarifa hiyo kutengeneza kwa umakini mkubwa mpango wa biashara ambao utakuwezesha kufikia malengo yako.
Mchakato wa kuandaa mchanganuo wa biashara utakuchochea kufikiria hata baadhi ya mambo ambayo usingekumbuka kuyafikiria katika hali ya kawaida. Mchanganuo wako utakuwa zana muhimu sana unapopambana kutafuta fedha kwa ajili ya biashara yako. Mchanganuo huo pia unaweza kutumika kama kigezo cha kila mara kufuatilia/ kupima mafanikio ya biashara yako.
Yako mambo kadhaa yanayohitajika katika biashara yoyote.
Jambo la kwanza kabla ya kuanzisha biashara ni kuwa unatakiwa ujiulize sababu za wewe kutaka kuingia kwenye biashara. Sababu zilizozoeleka za kuanza biashara ni:
Unataka kujiongoza mwenyewe.
Unataka uhuru wa kifedha.
Unataka uhuru wa kutumia ubunifu wako.
Unataka kutumia kikamilifu ujuzi na ufahamu wako
Jambo la pili ni kuamua biashara ipi inakufaa? Ili kufahamu ni biashara ipi inakufaa, jiulize maswali yafuatayo:
Ninapenda kutumiaje muda wangu?
Nimejifunza au kusomea ujuzi gani?
Watu wengine wanazungumzia ubora wangu kwenye mambo gani?
Nina muda kiasi gani kuendesha biashara kwa ufanisi?
Katika mambo ninayopendelea yapo ambayo yanaweza yakawa fursa ya biashara?
Biashara yangu itahudumia sehemu/ kundi gani katika soko?
Je? Wazo langu linatekelezeka na litakidhi hitaji katika soko?
Ushindani nilionao ni upi? Nami nina uwezo gani katika ushindani?
Biashara yangu ina manufaa gani kuzidi zingine zilizopo?
Je? Naweza kutoa huduma zenye ubora zaidi?
Je? Naweza kutafuta soko kwa ajili ya bidhaa/ huduma zangu?
Ukishapata majibu ya maswali hayo hapo juu ni wazi kuwa utakuwa ulishaanza kujua ni biashara gani unaweza kuianzisha. Lakini pia unatakiwa ujiulize maswali haya hapa ili kuwa na uhakika na biashara ambayo utaifanya.
Ninakusudia kuanzisha Biashara gani?
Nitauza bidhaa gani au nitatoa huduma gani? Biashara nitafanyia eneo gani?
Nitatumia ujuzi na uzoefu gani kwenye biashara?
Biashara yangu itakuwa na muundo gani kisheria?
Niiite biashara yangu jina gani?
Nitatumua vifaa gani, na nitakuwa na mahitaji gani?
Nahitaji bima ya aina gani?
Nahitaji fedha kiasi gani?
Nina rasilimali zipi?
Nitajilipaje?
Majibu yako yatasaidia kutengeneza mpango makini, uliofanyiwa utafiti wa kutosha, ambao utautumia kama ramani ya kuelekeza kila hatua katika utekelezaji wa biashara na hata kupata mtaji.
Chagua muundo sahihi wa biashara yako.
Unapoanzisha biashara yoyote, mojawapo ya maamuzi muhimu sana ya kufanya ni uchaguzi wa muundo wa hiyo biashara. Mambo yanayozingatiwa katika kuchagua muundo wa biashara ni pamoja na:
Masharti ya kisheria
Uwajibikaji wa wamiliki kwa madeni ya biashara
Aina ya shughuli za biashara
Mgawanyo wa mapato
Mahitaji ya mtaji
Idadi ya wafanyakazi na utawala
Manufaa na hasara za kihasibu/ kikodi
Urefu wa mzunguko wa biashara

SIRI YA UTAJIRI
Kwa ushauri wa kibiashara wasiliana na 0766865041,joseph
Watu wengi wanajiuliza, "Siri ya utajiri ni nini?" Jee ni mbinu gani
zinaweza kumsaidia mtu kupata utajiri? Siri kubwa ya utajiri ni
kujifunza elimu ya namna ya kutafuta mtaji, kuwekeza kwa busara kwa
namna ambayo daima panakuwa na ziada na faida. Kwa bahati mbaya
sana, elimu hii haifundishwi darasani ila wanayo wafanyabiashara
wachache na kila anayefanikiwa kujifunza siri hii huwa tajiri na
huendelea kuificha.
Kwa bahati nzuri, katika utafiti wagu nimeweza
kuigundua siri ya utajiri. Kwa kuwa ninapenda wasomaji wangu waweze
kufanikiwa na wapate manufaa kwa kununua kitabu hiki nimeamua
kuiweka siri hii wazi:-
- Siri ya kwanza ya kuelekea ukwasi ni kubuni mradi endelevu,
yaani unaoweza kuitoa ziada na faida.
- Siri ya pili ya kuelekea kwenye utajiri ni kujifunza na
kujenga tabia ya kuweka akiba
- Siri ya tatu ni kuwekeza fedha hizo za akiba katika vitega
uchumi ambavyo vinazalisha faida endelevu.
- Siri ya nne ni kujifunza namna ya kufanya biashara na
kuanzisha biashara yako ili iwe indelevu.
Kuna njia mbili za namna ya kupata utajiri zenye uhakika. Njia ya
kwanza ni njia ndefu ambapo wataalamu na watafiti wa masuala ya
fedha wameigundua njia hii ni rahisi kuifuata kwa sababu haihitaji
uwe na kipato kikubwa, wanashauri kwamba ujenge tabia ya kuweka
akiba, anza kuweka akiba ya T.shs 1,000 kila siku sawasawa na TShs
30,000 kwa mwezi, matokeo yake ni kwamba kama utaweka akiba yako kwa
kipindi cha miaka 65 bila riba yoyote utakuwa na akiba TSshs
23,725,000 (Milioni Ishirini na Tatu Mia Saba Ishirini na Tano
Elfu).
Kama utawekeza fedha hiyo na kupata riba ya asilimia 10% kwa
kila mwaka itazaa na kukuletea TShs 2,750,000,000 (Bilioni Mbili na
Milioni Mia Saba Hamsini). Hesabu hii inaweza ikakutisha na usiamini
macho yako lakini hiyo ni siri ya nguvu ya hesabu na riba kama
alivyozielezea mwanafizikia Enstein kwamba katika dunia hii hakuna
kitu chenye nguvu kama hesabu za riba.
Pengine njia hii inaweza kuwa
ni ndefu sana na ya kukatisha tamaa. Wengi wetu hatuwezi kusubiri
muda mrefu. Hivyo tungependa kuwa na mafanikio ya kiuchumi kwa
haraka. Lakini nasisitiza kama kipato chako ni kidogo anza leo
kuweka akiba ya TShs 1,000 kwa siku.
Dundulizo la akiba hii hukutiririshia utajiri bila wewe kukusudia
kwani utaweza kukidhi hitajiko la ghafla kama kuugua safari ya
dharura gharama za likizo na hata kutumia mbinu hii kama mpango wa
elimu kwa watoto wako iwapo utawaanzishia hivi mara tu kila
mmojawapo anapozaliwa au unaweza kuutumia kama upanga wa siku zijazo
kwa mirathi ukianza hivyo leo kwa kupangilia namna hiyo kwa kila
kusudio lako la baadaye.
Hebu tuangalie njia ya pili.
- Njia ya pili ya mkato ni kuongeza kiwango cha kuweka akiba kama
wewe ni mtu mwenye shughuli za kuzalisha ziada. Kipato chako
kinaweza kuwa kinaongezeka kila mara. Badala ya kuweka akiba ya TShs
1,000 kwa siku jiwekee malengo ya kuweka akiba ya TShs 10,000.
Anza kwa kutenga asilimia 10% ya mapato yako hadi utakapofikia lengo la
TShs 10,000 au zaidi kwa siku. Badala ya lengo lako kutimia kwa
miaka sitini na tano (65) litatimia haraka zaidi. Kwa mfano ukiweka
akiba ya TShs 10,000 kwa siku kwa muda wa miaka sita na miezi sita
bila riba yoyote utapata TShs. 23,725,000. Ukiwekeza fedha hiyo na
kupata riba ya asilimia 10% kwa miaka sita na miezi sita utapata
TShs. 33,917,505.78. Kama fedha hiyo utaendelea kuweka akiba kwa
riba hiyohiyo hadi kufikia muda wa miaka kumi utapata TShs.
63,112,201.43.
Kwa kuwa kitu cha muhimu hapa ni kuweka akiba na kuwekeza akiba hiyo
katika kitegauchumi chenye kutoa faida kubwa, utajiuliza jee uwekeze
kwenye kitega uchumi chenye kutoa faida kiasi gani? Wataalamu wa
mambo ya fedha wanashauri kuwa uwekeze fedha yako kwenye
kitegauchumi chenye kutoa faida ya angalau asilimia 10% Kwa mfano
unaweza kuwekeza kwenye Akaunti ya TAJIRIKA ya Standard Chatered
Bank" inatoa riba ya asilimia kumi 10% pia unaweza kuwekeza kwa
kununua hisa katika soko la hisa na mitaji.
Kwa wastani wa watafiti wa masuala ya fedha viwango vya mapato
yatokanayo na hisa kwa gawio pamoja na kukua kwa mtaji ni zaidi ya
asilimia 11% ambayo ni makubwa kwa kiwango cha kawaida cha asilimia
kumi (10%).
Baada ya kueleza siri ya namna ya kupata utajiri nitazitaja njia
zingine ambazo zinaweza kukuwezesha kuwa tajiri.
1. Unaweza kurithi mali na fedha kutoka kwa wazazi wako. Hii ni
njia ya kubahatisha kwani watu matajiri siyo wengi na hivyo watoto
wenye bahati kama hii ni wachache pia.
2. Unaweza kusomea ujuzi au utaalamu katika fani yenye malipo
mazuri na kujiajiri mwenyewe. Kwa mfano, unaweza kusomea fani kama
ya Uanasheria, Uhasibu na Udaktari au ufundi / sanaa na kadhalika.
3. Unaweza kuanzisha biashara yako na kuiendesha ili kupata
ziada kubwa.
4. Unaweza kuendeleza vipaji vyako na kuwa mwanamichezo au
msanii wa kulipwa.
5. Unaweza kutunga vitabu juu ya suala lolote unalolijua. Kwa
mfano, kama wewe ni mtu uliyebobea katika masuala ya muziki unaweza
kutunga kitabu kinachofundisha watu namna ya kuwa mwanamuziki.
Watunzi wengi wa vitabu ni matajiri wakubwa. Hii ni kazi unayoweza
kuifanya mara moja lakini ukavuna matunda yake kwa muda mrefu sana.
6. Unaweza kuwa mbunifu na kuanza kuuza mawazo yako au kutumia
chombo ulichokibuni kukuingizia fedha.
7. Unaweza kucheza bahati nasibu na kushinda. Tatizo hapa soko
na wateja wa aina hii ya huduma ni haba. Hiki ni kitu cha
kubahatisha na nimekitaja makusudi ili kuwapa onyo wasomaji kwani
watu wengi wanapenda sana kucheza michezo ya kubahatisha.
Uwezekano wa kutajirika kwa njia hii ni mdogo sana.
Hivyo,
nawashauri wasomaji kuachana na njia hii ya kutafuta utajiri.
Nawashauri wachague njia yoyote inayofaa na inawezekana kwa
kufuatana na mazingira yanayomzunguka mtu husika. Mkulima au mfugaji
anaweza kuzingatia fani hii na kutajirika sana. Kwa kweli hakuna
mipaka, hasa hapa kwetu Tanzania kwa sababu ya wingi wa fursa za
kuweza kujishughulisha na kuwa tajiri.
Maelezo ya kina juu ya aina ya biashara au mbinu unaweza kuzitumia
kutafuta na kupata faida utayapata katika sehemu ya pili ya kitabu
hiki.
Inawezekana kuwa tofauti kati ya mtu tajiri na mtu maskini inatokana
na kile tulichojifunza kutoka kwa wazazi wetu. Wazazi maskini
huwaambia watoto wao wajitahidi kusoma sana ili wapate maksi nzuri
darasani na ili baadaye waweze kupata kazi nzuri. Wakati wazazi
matajiri huwapa watoto wao elimu ya namna ya kutafuta fedha.
Kwa kawaida tukiwa shuleni tunapewa ripoti ya masomo. Katika maisha
tunatakiwa kuwa na ripoti yetu ya maisha nayo ni orodha ya mali
tulizonazo ikiwa ni pamoja na elimu ya kuzaliwa na ya kusomea na
fedha taslimu zile zilizo katika hifadhi mbalimbali.
Kwa kufuata tafsiri ya Umoja wa mataifa mtu masikini ni yule ambaye
kipato chake hakizidi TShs 1,000 kwa siku.
Inawezekana kuwa mfumo wa kifedha wa mtu maskini ni mfumo ambao
humfanya kutumia kipato chake chote kulipia matumizi huwa hana ziada
wala uwezo wa kuweka akiba hana madeni na hana mali.
Mfumo wa fedha wa mtu mwenye kipato cha kati ni mfumo ambao humfanya
kuwa na mali kama magari, nyumba na kadhalika. Mara nyingi mali hizo
huwa zinapatikana kwa mikopo na hutumia mshahara kulipia matumizi
na madeni, hasa kama madeni ni makubwa, mtu mwenye kipato cha kati
anapaswa kumuona mshauri wa maswala ya biashara.
Hatua anazoweza kuchukua ili kujikwamua na tatizo la madeni anaweza kulazimika kuuza
baadhi ya mali zake ambazo amezinunua kwa kutaka kuonyesha ufahari
tu na ambazo hazina umuhimu. Kwa mfano kama mtu ana magari matatu ya
kutembelea, anaweza kuuza magari mawili kubaki na gari limoja na
fedha atakayoiokoa kuiwekeza au kutumia kama mataji na kuanzisha
biashara ili kujiongezea kipato.
Mfumo wa mtu tajiri ni mfumo ambao unamwezesha kuwa na biashara
yake, kumiliki mali nyingi, kuwa na fedha nyingi katika akiba na awe
ameziwekeza kwenye vitega uchumi vinavyolipa faida kubwa zaidi ya
asiliamia kumi, kama vile nyumba za kupangisha na hisa. Mtu huyu
hana wasiwasi na maisha. Anaweza kusafiri au kuugua lakini
vitegauchumi vyake vinaendelea kumwingizia fedha. Siri kubwa ya
matajiri ni uwezo wa kutumia fedha na kuziwekeza kupata faida kubwa.
Hiki ni kitabu cha vitendo. Yote unayoyasoma humu inabidi uyafanyie
kazi ili yakusaidie. Tofauti kati ya maskini na tajiri iko katika
kuchukua hatua. Tajiri hujifunza mambo ya kumwendeleza na kuchukua
hatua kwa kutekeleza kwa vitendo yale anayojifunza na anayoyaona
yanaweza kumuinua kiuchumi. Maskini huwa anajifunza mambo na
kuyaacha kichwani bila kuchukua hatua au kuyafanyia kazi
aliyojifunza na hivyo fursa ya kupata utajiri inampita hivihivi. Kwa
hiyo, kama unataka kuwa tajiri anza mara moja kufanya yafuatayo:-
1. Anza kuweka akiba ya T.Shs 1,000 kila siku. Tengeneza
kisanduku na tumbukiza TShs. 1,000 kila siku. Zikifika TShs. 50,000
kafungue akaunti ya TAJIRIKA, kwenye Benki ya "Standard Chatered".
Kisha endelea kuweka TShs. 30,000 kila mwezi. Jinsi mapato yako
yatakavyokuwa yanaongezeka tenga asilimia kumi (10%) ya mapato yako
uweke akiba kila mwezi.
Lengo lako liwe ni kuweka TShs 10,000 au
zaidi kila mwezi. Fedha unayoweka ni kama unapanda mbegu. Kumbuka
hii ndiyo hatua ya kwanza kuelekea kwenye utajiri. Faida katika
benki hii ni kubwa. Inaanzia asilimia 6.5% kwa kianzio cha TShs.
50,000 hadi TShs. 5,000,000 na asilimia 10% kwa kiwango kinachozidi
TShs. 10,000,000. Fedha utakazoziweka huko usiziguse mpaka ukiona
zimekuwa nyingi ndipo utaamua na kupanga ukaziwekeze sehemu gani.
2. Jifunze pia mbinu za kutafuta fedha.
Njia rahisi ni ya uhakika ya kukuwezesha kufanikiwa kiuchumi katika maisha ni kutafuta
mshauri au mtaalamu anayejua mbinu za uongozi wa biashara ili
akushauri vizuri juu ya yale unayonuia kutekeleza.
3. Inawezekana pia bado hujawa na biashara ya aina yoyote.
Kama ndivyo anza kufanya utafiti kuona utafanya biashara gani.
Mawazo ya biashara gani ufanye unaweza kuyapata katika sehemu ya
pili ya kitabu hiki. Kila mara hakikisha unatenga asilimia 10% ya
mapato yako na kuweka kwenye akaunti yako ya TAJIRIKA. Kumbuka
kwamba kuwa na biashara yako ni siri ya pili ya kuelekea kwenye
kupata utajiri. Kama unayo biashara yako unaweza kumtafuta mtaalamu
wa biashara kuangalia jinsi unavyoweza kuiboresha au kuipanua.
4. Panga malengo ya muda wa mwaka mmoja miaka mitano na miaka
ishirini ili kuhakikisha kwamba unajikomboa kiuchumi. Malengo yako
makuu yawe ni:- kuwa na akiba ya fedha za kutosha katika akaunti
yako , kuwa na biashara yako, na vitega uchumi vya aina tofauti
ambavyo unaweza kuvisimamia vizuri.
5. Kama wewe ni mwajiriwa, kipimo chako cha mafanikio kiwe ni
kujiuliza swali, kama utaacha kazi yako ya mshahara utaweza kuishi
kwa kutumia kipato chako cha pembeni kwenye biashara yako kwa muda
gani? Mafanikio yako yatakuja pale utakapoweza kutumia kipato chako
cha ziada bila kutegemea mshahara, na hapo ndipo unaweza kuacha kazi
na kwenda kuimarisha biashara zako au kuendelea na kazi huku pia
ukijiimarisha kibiashara.
6. Kama utafuata mpango wa namna hii na kujituma kwa juhudi na
maarifa kwa muda wa miaka mitano (5) unaweza kuwa tajiri na maisha
yako yanaweza kuwa mazuri.

SIFA ZA MTU ANAYETAKA KUANZISHA BIASHARA
Nidhamu binafsi – Hakuna mjasiriamali anayependa kuona biashara yake inakufa, kila mmoja analenga kuhakikisha biashara inafanikiwa na huondosha kila jambo linaloweza kuhatarisha ustawi wa biashara husika. Wajasiriamali waliofanikiwa wana nidhamu ya kuchukua hatua kila siku kuelekea kwenye kufanikisha malengo yao. Hakikisha unanidhamu ya kutunza mda na nidhamu ya kutumia pesa zinazopatikana kutokana na biashara yako.
Kujiamini – Mjasiriamali hupaswi kuwa na wasiwasi kuwa unaweza kufanikiwa au la, unapaswa kujiamini mda wote kuwa utafanikisha biashara yako. Jitahidi kudhihirisha kujiamini huko kwa kufanya kazi kwa bidii ili kifikia malengo uliyojiwekea.
Muwazi wa fikra – Mjasiriamali anatambua kuwa kila tukio au hali ni fursa ya kibiashara. Mawazo mapya yanaibuliwa kila mara kuhusu mtiririko wa kazi na ufanisi, ujuzi, na biashara mpya. Mjasiriamali ana uwezo wa kutizama kila jambo [hali/ tukio] linalomzunguka na kulitumia kufanikisha lengo lake.
Muanzilishi – Mjasiriamali anafahamu kuwa kama kuna jambo linalopaswa kufanyika basi yeye mwenyewe ndiye anayepaswa kulianzisha. Hujiwekea vigezo na kuhakikisha biashara inafuata kuelekea kutekeleza/ kukidhi vigezo hivyo. Wako makini katika kutwaa fursa bila kuhitaji kusubiri mtu mwingine awape fursa
Mshindani – Chanzo cha biashara nyingi ni mjasiriamali mmoja kutambua kuwa anaweza kufanya biashara hiyo kwa ubora kuliko mwingine/ wengine. Wajasiriamali wanahitaji kufanikiwa katika biashara wanazoanzisha mithili ya mchezaji anavyohitaji kushinda katika mchezo anaocheza. Mjasiriamali ni mwepesi kuonesha namna taasisi yake ilivyofanikiwa katika hatua mbalimbali.
Mbunifu – mojawapo ya mambo muhimu katika ubunifu ni kumudu kuunganisha mambo ambayo hayaonekani kuwa na uhusiano katika kutengeneza fursa. Wajasiriamali huja na suluhisho baada ya kuchambua na kutengeneza uhusiano wa hali/ matukio mbalimbali. Huweza hata kubadili malengo ya bidhaa fulani na kuiuza katika soko tofauti.
Kutokata tamaa – Wajasiriamali hawakatishwi tamaa na kushindwa. Kila anaposhidwa huichukulia kama fursa ya kujifunza na kufanikiwa. Wanatamani kila wanalofanya lifanikiwe, hivyo hujaribu tena na tena hadi wafanikiwe. Hawaamini kuwa kuna jambo lisilowezekana
Ujuzi binafsi – Mjasiriamali ana ujuzi mzuri wa kuwasiliana katika kuuza na kuwapa motisha waajiriwa wao. Wajasiriamali wengi waliofanikiwa hufahamu namna ya kuwapa motisha waajiriwa wao hivyo kukuza biashara zao. Ni wazuri katika kuelezea faida za hali mbalimbali na kuwafundisha wengine katika kufanikiwa.
Mwenye kuheshimu maadili ya kazi yake – Mjasiriamali hufanikiwa kwa kufuata/ kutii kanuni na taratibu zilizowekwa na mamlaka husika. Mifano ya wajasiriamali wasio na maadili ni: Muuzaji wa matunda anayeokota matunda kutoka kwenye shimo la taka kwa ajili ya kuwatengenezea wateja wake sharubati (juisi), au mjasiriamali anayeuza nyama isiyokaguliwa au iliyokatazwa kwa matumizi ya binadamu.
Mwenye kupenda kazi yake – Kupenda na kuthamini kazi yake ni sifa muhimu kuliko zote anayohitaji mjasiriamali ili kufanikiwa. Mjasiriamali ana mapenzi ya dhati kwa kazi yake. Yuko tayari kufanya kazi saa za ziadakuhakikisha biashara yake inafanikiwa, maana hupata furaha kuona biashara inafanikiwa. Mjasiriamali anayefanikiwa ni yule ambaye hujifunza bila kuchoka na kutafiti namna mbalimbali za kufanya biashara yake iwe bora zaidi.
Wajasiriamali wanaofanikiwa hutizama biashara zao kama mtu aliye juu ya kilima na kuona biashara yake ilivyo. Akishaiona, anataka kwenda mbali zaidi. Wanafahamu namna ya kuzungumza na waajiriwa wao, na biashara zao hutanuka kwa sababu hiyo.

KWA USHAURI ZAIDI WASILIANA NASI KWA 0766865041
Je, Unahitaji Kufanya Biashara Na Hujui Ni Biashara Ipi Ya Kufanya? Soma Hapa Kujua Ni Biashara Ipi Ya Kuifanya Sasa
Wapo watu ambao mara nyingi hujiuliza ni biashara gani wafanye katika maisha yao ambayo itaweza kuwaingizia pesa nyingi ya kutosha. Ni wazo ambalo hutokea kutokana na pengine kuona kila biashara wanayoitazama kwa wakati huo kama hailipi. Hali hiyo husababisha mkanganyiko mkubwa wa mawazo ambao husababisha wabaki njia panda.
Kama imeshawahi kukutokea hali kama hii kwa namna moja au nyingine makala hi ni muhimu sana kwako kuisoma. Kwa kusoma makala hii inakuonyesha kwa uwazi orodha za biashara ambazo unatakiwa uzifanye ukiwa katika mazingira uliyopo. Karibu kila biashara ipo hapo, kazi ni kwako kuchagua mojawapo unayoipenda na kuifanya, acha kulalamika tena kuwa huelewi nini cha kufanya.
Twende kwa pamoja kuzijua biashara hizo ambazo unauwezo wa kuzifanya na kukufikisha kwenye mafanikio makubwa:-
1. Kutengeneza na kuuza chaki
Hii ni moja ya biashara nzuri unayoweza kuifanya na soko lake liko juu. Unaweza ukanunua mashine yako za kutengeneza chaki na kisha ukaanza kuzisambaza kwenye stationary au mashuleni. Uzuri wake mashine hizi za kutengenezea chaki gharama yake pia sio kubwa sana ni ya kawaida tu ambayo hata wewe unaweza kuimudu. Hii inaweza ikawa ni sehemu mojawapo ya kuingizia kipato chako.
2. Kufungua duka la kuuza asali
Uzuri wa bidhaa hii muda mwingi soko lake lipo juu. Ni biashara ambayo unaweza ukaifanya kwa kuagizia asali kutoka kwa wakulima kama nilivyo mimi na kisha kuanza kuiuza moja kwa moja katika vipimo vinavyotakiwa.
Kama huwezi kufungua duka hili unaweza ukafanya mbadala wake ukaenda kutengeneza mizinga wewe mwenyewe na kuwafuga. Pia hii ni biashara ambayo ni nzuri kwako kukuingizia kipato kikubwa kwa urahisi.
3. Kuanzisha biashara ya kuuza vyakula katika matamasha mbalimbali
Hapa siyo lazima uwe na Hotel au Mgahawa ndiyo uanzishe biashara ya namna hii. Kikubwa unahakikisha unakuwa makini na sherehe katika eneo ulilopo. Kama ni kuweka mawakala watakao kusaidia kukujulisha kuwa eneo fulani kuna sherehe ya aina fulani na siku fulani itakuwa nzuri zaidi kwako kuchangamkia tenda hizo mapema.
4. Kujenga nyumba za kulala wageni
Kama mtaji wako unaruhusu hii ni moja kati ya biashara nzuri kuifanya. Ni biashara ambayo hahitaji kukimbizana sana ukishamaliza kujenga, zaidi unatakiwa kuweka mfumo sahihi wa kusimamia na kuanza kuingiza pesa. Na kwa bahati nzuri kwa Tanzania yapo maeneo mengi ambayo yanauhitaji mkubwa wa huduma hii. Ni Biashara nzuri kuifanya hata kama umri umeenda, kwa sababu haihitaji mkimbizano mkubwa.
5. Kutengeneza matoroli/mikokoteni na kuikodisha
Katika hili hapa unatakiwa kutengeneza kwa idadi unayoitaka na unamwachia kijana ambaye anaikodisha huku ukiendelea na majukumu mengine. Unaweza ukaiona ni biashara ndogo lakini fuatilia kwa waliowekeza nguvu na mawazo yao hapo wakwambie kile wanachokipata utashangaa.
6. Kuazisha huduma ya AIRTEL MONEY, MPESA, TIGOPESA, EZYPESA
Hakuna ubishi hii ni moja ya huduma ambayo imezagaa kila eneo na watu wengi wanaihitaji. Kikubwa ni juhudi yako na kuzingatia eneo uliloweka biashara yako liwe hasa la mzunguko mkubwa zaidi kukuwezesha kufanya biashara hii vizuri.
7. Kupamba maharusi na kumbi za harusi/sherehe
Pia unaweza ukajiingiza hapa na kushughulika na kupamba tu maharusi. Kama hujui sana ni kitu cha kujifunza pia, kisha unachangamkia sherehe zinazojitokeza mjini.
8. Kuanzisha kilimo cha kisasa
Wengi wanaposikia kilimo kichwa kinakataa. Lakini ikiwa utawekeza kwenye kilimo cha kisasa na cha kitaalamu ambacho unategemea kumwagilia zaidi, uwe na uhakika unatoka. Yapo mazao mengi unaweza ukalima lakini mojawapo ni kitunguu. Inaweza ikawa ni njia rahisi ya kufikia mafanikio yako kuliko unavyofikiri.
9. Mashine za kusaga na kukoboa nafaka
Pia unaweza ukajitengenezea kipato chako na kuwa kikubwa na cha uhakika kwa kufunga mashine hizi. Kila siku watu wanahitaji kula hivyo ukifunga mashine hizi ni rahisi sana kupata wateja wa kuwauzia unga na kupata faida. Na uzuri mahindi ya kusaga yanapatikana maeneo mengi kwa wingi kama kule Kibaigwa (Dodoma), Gairo(Morogoro), Kiteto(Manyara) na maeneo mengine mengi kama Iringa na mbeya.
10. Yadi kwa ajili ya kupaki magari
Kitu unachotakiwa hapa ni kununua kiwanja na kukigeuza kuwa yadi ambapo magari yanakuwa yanapaki iwe kwa kulala au kwa muda. Kila gari linalokuwa linapaki linakuwa linatozwa kiasi fulani cha pesa ambacho kinakuwa ndiyo hiyo huduma unayoitoa.
Zipo aina nyingi sana za biashara ambazo unaweza ukazifanya na kukuingizia kipato. Katika Orodha ya kipande cha makala hii kinachoendelea zimebaki biashara zaidi 100 ambazo sijaziweka hapa kutokana na ufinyu wa nafasi. Kuzijua zinazoendelea na ufafanuzi wake unaweza ukaniandikia email kwenda josephmwaselela@gmail.com nitakutumia mara moja.
ILA KAMA YOTE HAYO UTASHINDWA KUPATA LA KUFANYA WEWE UTAKUWA UMESHAPOTEA, ENDELEA NA UTARATIBU WAKO WA KUILAUMU SERIKALI.
Tunakutakia ushindi katika safari yako ya mfanikio, ila kumbuka daima tupo pamoja mpako maisha yako yaimarike.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
joseph
0766865041
Wednesday, 25 January 2017
NMB YAIBUKA KIDEDEA
BENKI ya NMB imewekwa katika daraja la kwanza na kampuni ya kimataifa ya utafiti ya Moody’s Investors Service kwa uwezo wake wa kuhimili madeni na usalama wa kifedha.
Kampuni hiyo ya Moody’s ni moja ya kampuni zinazofanyia tathmini na kushindanisha utendaji wa taasisi za fedha duniani.
Kwa mujibu wa taarifa ya benki hiyo ya NMB kwa waandishi wa habari Dar es Salaam jana, daraja hilo linaifanya benki hiyo kuwa ni benki inayoongoza kwa kuwa na huduma bora na za uhakika katika nchi za Afrika isipokuwa Afrika Kusini.
“Benki hii imepata daraja hili baada ya kufanyiwa tathmini katika maeneo mbalimbali ikiwemo mazingira ya uendeshwaji wake, mazingira ya jumla pamoja na shughuli za kibiashara za benki hii,” ilisema taarifa hiyo ya benki.
Kupatikana kwa daraja hilo, kunaendana na malengo ya NMB ya kuhakikisha benki hiyo inakuwa ni taasisi ya fedha inayoongoza kwa kutoa huduma bora nchini.
Aidha, daraja hilo, linaonesha namna pia benki hiyo ilivyo imara na yenye akiba ya kutosha, lakini pia inayozingatia suala la utawala bora.
Bodi ya Wakurugenzi na menejimenti ya benki hiyo, imefurahishwa na kitendo cha benki hiyo kupatiwa daraja hilo, kwani kutaisaidia NMB kuwa katika nafasi ya kujadili masharti mazuri zaidi na watoa mikopo.
MAMBO 9 YALIYO ISHANGAZA DUNIA KWA JINSI YALIVYOTOKEA.
1. Ozil na Ferrari
Enzo Ferrari mwanzilishi wa ferrari ambaye Kisura anafanana na Mchezaji wa mpira Mesut Ozil alifariki Mwaka ambao Ozil alizaliwa.
2. Lincoln na Kennedy.
Maraisi wawili wa Marekani waliowahi kupendwa sana Lincoln na Kennedy wote walikuwa na urefu sawa wa futi sita. Wote waliwahi kwenda vitani kabla ya kuwa Marais. Wote walikufa siku ya ijumaa. Wote kwa kupigwa risasi kichwani. wote wakiwa wamekaa pembeni ya wake zao.
3. Kutabiriwa kwa Titanic.
Miaka 14 kabla ya kutengenezwa titanic, mwandishi wa vitabu Morgan Robertson alitabiri Kuzama kwa Titanic. Kwenye kitabu chake cha Futility, or the Wreck of the Titan alitumia jina la titan kusimulia meli isiyoweza kuzama. Meli ya kwenye kitabu ilikuwa urefu sawa na meli ya ukweli ya Titanic. Meli ya kwenye kitabu cha Robertson ilizama kwa kugonga mwamba wa barafu kwenye Bahari ya Atlantic ya kaskazini, kitu ambacho kilitokea pia kwenye titanic ya ukweli.
4. Mfalme Umberto I wa Italy
Mfalme Umberto I wa Italy alifahamiana na mumiliki wa mgahawa baada ya kugundua kuwa wote wamezaliwa siku moja, mji mmoja na wote wameoa wanawake wenye majina yanayofanana. Siku chache baadaye wote wakauliwa siku moja sehemu tofauti kwa kupigwa risasi.
5. Napoleon na Hitler (129).
Adolf Hitler alizaliwa miaka 129 baada Napoleon Bonaparte. alitawala miaka 129 baada ya utawala wa Napoleon. aliivamia Urusi miaka 129 baada ya Napoleon kuivamia Urusi pia. Na aliondolewa madarakani miaka 129 baada ya Napoleon naye kuondolewa madarakani.
6. Gari la Archiduke Ferdinand.
Kuuliwa kwa Archduke Franz Ferdinand kulifungua rasmi vita ya kwanza ya dunia. Gari alilokuwa amepanda wakati anauliwa lilikuwa na plate number A11-11-18. Vita vya kwanza vikaisha rasimi November 11, 1918 - 11-11-18.
7. Ujenzi wa Bwawa la Hoover
Ujenzi wa bwawa hili liligharimu maisha ya watu wengi, lakini mtu wa kwanza kufa ni bwana J.G. Tierny, ambaye alifariki December 20, 1922. Mfanyakazi wa Mwisho kufa kwenye huu ujenzi alikuwa Mtoto wa Tierny alikufa siku sawa na siku aliyokufa baba ake miaka 13 baadaye, December 20, 1935.
8. Video game Iliyotabiri semptember eleven (Twin tower iliyopigwa na Osama)
Video game ya Deus Ex ambayo ilikuwa officially released June 2000. Game hili lilitengenezwa kuakisi maisha ya New york city, lakini katika hatua za mwisho kabisa wakagundua kwamba wamesahau kuyaweka majengo pacha ya biashara (Twin Towers). Ili kukwepa gharama na muda wa kuanza kutengeneza upya ikabidi waandike tu mwanzo wa game kwamba yale majengo yamelipuliwa na magaidi.
9. Ndugu wawili wa Hamilton
Dereva wa baiskeli yenye injini (Moped) mji wa Hamilton, Bermuda alifariki mwaka 1974 kwa kugongwa na taxi. mwaka ulifuta 1975 eneo lile lile, mdogo wake naye aligongwa akiwa anaendesha baiskeli ya injini, gari iliyomgonga ni ile ile iliyomgonga kaka ake, na cha ajabu kabisa dereva yule yule, na pia alikuwa amebeba abiria yule yule aliyekuwa amemubeba siku anamugonga kaka mtu.

![https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiL38MljhrGli_cK4lBol_RRjhE7LyyFbjYWm4Y-KCE328UC1MWmIMiCt17Ex8wyIUTXraXQXXIpR1YJGgeyEKbbcW0JjFvd-nKRJooNXOHKM9t_9FAD-r8SpssHnJ3SnN2w37J7BlJVrTW/s320/](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiL38MljhrGli_cK4lBol_RRjhE7LyyFbjYWm4Y-KCE328UC1MWmIMiCt17Ex8wyIUTXraXQXXIpR1YJGgeyEKbbcW0JjFvd-nKRJooNXOHKM9t_9FAD-r8SpssHnJ3SnN2w37J7BlJVrTW/s320/d73d7446-4194-4ae4-a8a5-716959e833e5.jpg)
Tuesday, 24 January 2017
TARATIBU ZA KISHERIA ZA UANZISWAJI WA BIASHARA YOYOTE.
Kupitia ukurasa huu, napenda kuufahamisha umma, hasa kwa wale wenye njozi ya kuanzisha biashara mpya kwenye ardhi ya Tanzania. Yaweza kuwa mojawapo kati ya biashara zifuatazo, yaani biashara ya mtu binafsi (sole proprietorship), biashara ya Ubia (partnership) na biashara za makampuni.
MMILIKI BINAFSI (SOLE PROPRIETORSHIP)
Kwa wamiliki binafsi wa biashara wazawa au wageni wanahitaji kuwa na vitu vifuatavyo:
- TIN - Leseni ya biashara
.....TIN inatolewa bure na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), hakuna usumbufu katika upatikanaji, inaweza kuchukua siku 1 hadi 2. Jambo la msingi ni kwamba mlipa kodi ni lazima afike ofisi za TRA ili kujiandikisha kupitia biometric scanning inayohusisha kuchukuliwa picha, alama za vidole na sahihi....
-Akaunti katika benki ya biashara
Kwa mtu ambaye sio raia wa Tanzania anapaswa kuwa na kibali kinachomruhusu kufanya biashara nchini kutoka Idara ya Uhamiaji. TIN ni kifupisho cha maneno Taxpayer Identification Number, kwa Kiswahili namba ya utambulisho wa mlipa kodi. Ni muhimu kwa mfanyibiashara yeyote kusajiliwa na kutambulika kama mlipa kodi kupitia mamlaka ya mapato Tanzania kwani TIN ni kama uthibitisho wa mfanyabiashara kutambuliwa na mamlaka na taasisi yoyote ya kibiashara kama vile mamlaka za miji zinazotoa vibali vya biashara pamoja na mamlaka ya mapato yenyewe. Huwezi kufanya biashara na taasisi kubwa kama vile kupewa uzabuni wa kusambaza bidhaa bila kuwa na TIN. Baadhi ya makampuni ya mawasiliano hutoa wakala kwa watu binafsi kutoa huduma za kutuma na kupokea fedha kupitia mitandao ya simu kama vile M-PESA, TIGO PESA, AIR TEL MONEY na mitandao mingine mingi. Moja ya vigezo vikubwa vya kupewa wakala wa mitandoa hii ni kuwa na TIN. Baadhi ya wafanyabiashara wanaochukua uwakala wa kampuni za simu ama kwa kufahamu au kwa kutofahamu wameunganishwa na wakala mwingine katikati na kuwafanya wao kuwa watu wa tatu. Hii inapunguza kamisheni ambayo wakala anapata kwa kuwa kuna sehemu ya malipo inayokwenda kwa huyu mtu wa kati. TIN inatolewa bure na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), hakuna usumbufu katika upatikanaji wa TIN.
TIN inaweza kupatikana ndani ya siku 1 hadi 2 kutegemeana na idadi ya maombi ambayo mamlaka imepokea kwa kipindi husika. Mlipa kodi ni lazima afike TRA ili kujiandikisha kupitia biometric scanning inayohusisha kuchukuliwa picha, alama za vidole na sahihi. Katika kukamilisha zoezi hili ni vema muhusika akafika moja kwa moja TRA. Siku hizi kwa ajili ya kugawana ridhiki, wapo watu wa kati wengi ambao husaidia kuwaunganisha waombaji wa TIN na TRA. Watu hawa hutumia ushamba wa watu wengi kujipatia sehemu ya kipato. Si mbaya sana kuwa nao lakini baadhi yao huwatoza wateja wao ujira mkubwa ambao hufanya zoezi la kuomba TIN kuwa na gharama kubwa wakati inaelezwa na mamlaka husika kuwa ni bure. Hata kama muombaji wa TIN atamtumia mtu wa kati ni muhimu yeyemwenyewe kuwepo ili kutoa ushirikiano atakapotakiwa kuchukuliwa picha na sahihi. Lakini pia kufika TRA kwa mfanyabiashara mpya ni muhimu ili kuweza kupata maelezo ya ziada yanahusiana na biashara mpya na msaada wa kitaalamu. Mfanyabiashara atapata fursa ya kuwauliza maafisa wa TRA maswali kadhaa kuhusu biashara kama vile ni kwa nini vipo vyombo vingine vinavyoweza kukamata au kuzuia mzigo unaposafirishwa kutoka duka la jumla, na nini afanye ili kuepukana na usumbufu kama huu? Ni kazi ya maafisa wa TRA kukujibu maswali yote hayo bila malipo kwani ni moja ya kazi walizoajiriwa kuzifanya. Kwa kujisajili kupata namba ya mlipa kodi inaonesha kuwa unatambua wajibu wako kama mfanyabiashara wa kuchangia pato la taifa kwa njia ya kulipa kodi. Na jambo hili ni jema tu kama alivyowahi kusema Arthur Vanderbilt "Taxes are the lifeblood of government and no taxpayer should be permitted to escape the payment of his just share of the burden of contributing thereto." Na Richard M. Nixonaliyesema “Make sure you pay your taxes; otherwise you can get in a lot of trouble.”
LESENI YA BIASHARA Unatakiwa kuwa na leseni ya biashara ambayo hupatikana katika ofisi za manispaa husika chini ya Sheria ya Leseni ya Biashara Sura ya 208 kifungu cha 3 ambacho kinasema ni marufuku kufanya biashara bila kuwa na leseni halali katika eneo halali. Muombaji wa leseni anatakiwa kufika katika moja ya ofisi ya afisa biashara katika wilaya au manispaa au mji au katika ofisi za wizara ambao ndio wanahusika na utoaji wa vibali vya biashara katika maeneo husika. Mtu yeyote raia wa Tanzania anayo haki ya kupatiwa leseni ya biashara ili mradi awe ametimiza umri wa miaka kumi na nane (18) mwenye akili timamu ambaye hajawahi kupatikana na kosa la jinai na awe na eneo la kufanyia biashara linalokubalika kisheria. Kwa mtu ambaye sio raia wa Tanzania anapaswa kuwa na kibali kinachomruhusu kufanya biashara nchini kutoka Idara ya Uhamiaji. Baada ya kujaza fomu na viambatanisho, maombi hupitishwa ngazi zinazotakiwa kisheria – Mpango Miji na Afya. Baada ya hapo leseni hutolewa ndani ya siku moja au mbili na si zaidi. Acaunti ya benki itamuwezesha mfanyabiashara kuhifadhi na kupokea fedha kama malipo dhidi ya washirika wake kibiashara.
2. BIASHARA YA UBIA (PARTNERSHIP)
Kwa watu wanaotaka kufanya biashara kwa kuingia ubia ni lazima wafanye kwanza usajili kwa msajili wa makampuni BRELA na kupewa cheti cha umiliki kinachoonesha idadi na majina ya wabia katika biashara husika na asilimia za uchangiaji katika biashara. Katika kuomba TIN wabia watatakiwa kuwasilisha nakala ya cheti cha usajili toka BRELA. Kila mwanachama katika biashara ya ubia atatakiwa kuomba TIN, ikiwa mmoja wao alikuwa nayo hatatakiwa kuomba tena.
3. MIFUKO YA DHAMANA
Mwenye dhamana anatakiwa kuomba usajili BRELA kwanza na kupewa cheti cha usajili kinachoonesha majina na anuani za wenye dhamana . Na pia kila mwanachama anatakiwa kuwa na TIN.
4. MASHIRIKA YA UTU
Taasisi hizi ni lazima zipate ukubali wa kujiendesha kutoka kwa kamishina. Maombi ni vema yakaambatanishwa na nyaraka ambatanishi kutoka wizara ya mambo ya ndani. 5. KAMPUNI Uanzishaji wa kampuni unahitaji kusajili jina la biashara kwa Wakala wa Usajili wa Biashara (BRERA; Business Regulatory and License Agency). Promota wa kampuni anatakiwa kuwasilisha kwa msajili kanuni za uendeshaji wa kampuni (memorandum and articles of association). Cheti cha ushiriki katika biashara toka BRELA kitaambatanishwa wakati wa kufanya maombi ya TIN pamoja na kanuni za uendeshaji wa biashara.
UTARATIBU WA KUPATA LESENI YA BIASHARA
Mwombaji anapaswa kujaza fomu ya maombi 9TFN kikamilifu na kuambatanisha kivuli cha:-
(i) Jina la Biashara kama sio mtu binafsi (Certificate of Incorporation or Registration).
(ii) “Memorandum and Article of Association” kama ni Kampuni
(iii) Kitambulisho cha mpiga kura, Cheti cha kuzaliwa au Hati ya kiapo kuonyesha kuwa ni
Mtanzania na Mgeni Hati ya kuishi nchini daraja la “A” (Residnece Permit Class “A”)
(iv) Hati ya kiuwakili (prowess of a Honey) kama wenye hisa wote wa Kampuni wapo nje ya nchi.
(v) Ushahidi wa maandishi kuwa ana mahali pa, kufanyia biashara (Kwa mfano hati za nyumba, mkataba wa upangishaji, risiti za malipo ya kodi za majengo au ardhi.
(vi) Hati ya kujiandikisha kama mlipa kodi TRA (TIN). Kwa leseni zinazodhibitiwa na Mamlaka mbalimbali , Kwa mfano (TFDA, EWURA, TAURA, CRB, TILLI) n.k lazima mwomaji kuwa na leseni husika kabla ya kuomba leseni ya biashara. Leseni hizi hutolewa kulingana na shughuli unayotaka kuifanya, kwa mfano kuna biashara zinalazimisha uwe na leseni kutoka Shirika la Viwango la Taifa (TBS), TFDA, Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Baraza la Wakala wa Usalama na Afya mahala pakazi (OSHA) na nyinginezo.
Utaratibu wa wajasiriamali wadogo na wa kati (smes) kuwezeshwa kupata alama ya ubora ya ‘tbs’ Serikali hutenga fedha kila mwaka kwa ajili ya kuhudumia wajasiriamali wadogo na wa kati pale wanapoomba bidhaa zao wanazozizalisha wenyewe zithibitishwe ubora. Katika utaratibu huu, wapo wajasiriamali ambao husamehewa kulipa ada yoyote kwa sababu ya mitaji yao kuwa midogo. Ili kupata msamaha huu, vigezo vifuatavyo huzingatiwa: Mjasiriamali hutakiwa kuwa na barua ya utambulisho kutoka ofisi ya SIDO iliyo karibu. Ni vema kuhakikisha kuwa barua inafafanua vizuri na kwa kina shughuli zinazofanywa. Kwa wale wanaozalisha vyakula huhitajika kuwa na taarifa fupi kutoka Idara ya Afya iliyo karibu na mahali pa uzalishaji au cheti cha TFDA. Mjasiriamali hupaswa kuwa na leseni ya biashara. Wajasiriamali waliokwishapata leseni ya kutumia alama ya ubora hupaswa kutunza rekodi za uzalishaji na mauzo ambazo watatakiwa kuzionesha kwa wakaguzi wa TBS pindi zinapohitajika.
HATUA ZA KUPATA ALAMA YA UBORA YA ‘tbs’
1. HATUA YA KWANZA – MAOMBI
Maombi ya uthibitishaji wa ubora wa bidhaa hufanywa na mwombaji kwenda kwa Mkurugenzi Mkuu wa TBS kwa maandishi. Majibu hutolewa yakielezea taratibu na gharama zote. Majibu huambatana na fomu maalum ambayo mwombaji huijaza na kuirudisha TBS ikiwa na viambatanisho vifuatavyo: Mtiririko wa uzalishaji wa bidhaa husika; Mfumo wa uongozi ukionyesha kitengo cha udhibiti ubora; Orodha ya malighafi anazotumia na mahali zinakotoka kwa kila bidhaa; Ramani inayoelekeza jinsi ya kufika kiwandani kwako; Baada ya hapo tarehe ya kufanya ukaguzi wa awali hupangwa.
2.HATUA YA PILI – UKAGUZI WA AWALI
Ukaguzi wa awali hufanywa na wakaguzi wa TBS wakati kiwanda kikiwa katika uzalishaji. Sampuli huchukuliwa na kupimwa ili kuona kama zinakidhi matakwa ya kiwango husika. Mkaguzi huandaa taarifa kuhusu hali halisi ya kiwanda na mambo yanayostahili kurekebishwa.
.
3 HATUA YA TATU – UPIMAJI Sampuli zilizochukuliwa hupimwa katika maabara za TBS kwa kufuata kiwango husika. Baada ya kazi ya upimaji kumalizika, ripoti ya maabara hutolewa kwa mwombaji.
4. HATUA YA NNE – UTOAJI WA LESENI Maamuzi kuhusu kutoa au kutotoa leseni ya kutumia alama ya ubora hutegemea tu ripoti ya ukaguzi wa awali wa kiwanda pamoja na ripoti ya maabara. Kimsingi ripoti zote mbili zinatakiwa kuonyesha kwamba mazingira ya uzalishaji kiwandani, mfumo wa uzalishaji na bidhaa iliyopimwa havina matatizo. Ikiwa sivyo basi mzalishaji hutakiwa kufanya marekebisho na baadaye mkaguzi wa TBS hutumwa tena na kuleta sampuli nyingine.
MUDA WA LESENI (VALIDITY OF LICENCE) YA ALAMA YA UBORA YA ‘tbs’
Leseni ya kutumia alama ya ubora ya ‘tbs’ hudumu kwa mwaka mmoja na huhuishwa (renewal) baada ya kuhakikisha kwamba taratibu zilizokubalika (Scheme of Inspection and Test, SIT) zinafuatwa. Biashara za sekta ndogo zinazojihusisha na uvunaji maliasili kama vile uchimbaji madini na madini ya ujenzi (mawe, kokoto, mchanga); uvuvi; kuni na uchomaji mkaa, hazihitaji kusajiliwa na BRELA, bali vibali na leseni zake hutolewa na sekta husika. b. Biashara katika sekta ndogo nyingine zote zinahitaji kusajiliwa na BRELA, yenye ofisi zake jijini Dar es Salaam. c. Kuna kundi la tatu la biashara, ambazo haziko rasmi, na hizi husajiliwa kwa kupewa leseni ya Nguvu Kazi. Leseni za Nguvu Kazi hutolewa na mamlaka za serikali za mitaa chini ya Sheria ya Maendeleo ya Rasilimali Watu, kwa lengo la kuzitambua biashara ndogo ndogo. Idara ya Maendeleo ya Jamii na Idara ya Maendeleo ya Ushirika katika ngazi ya halmashauri zinahusika tu katika kusajili vikundi vya wakulima na wafanyabiashara katika maeneo yao. Kampuni zote sharti zisajiliwe na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) au mamlaka nyingine inayoruhusiwa kisheria.
LESENI ZA VILEO
Sheria ya leseni za vileo imenyambulisha aina tisa za leseni za vileo zinazoweza kutolewa chini ya sheria hii: Retailers On Leseni hii humruhusu mwenye biashara kuuza pombe na kunywa eneo la biashara RETAILERS OFF Leseni hii haimruhusu mtu kinywea pombe eneo la biashara bali kwa watu wanaochukua kunyewea majumbani (Take away) kama Groceries. WHOLESALE Leseni hii ni kuuza pombe kwa jumla HOTEL Leseni hii humruhusu mwenye leseni kuuza pombe kwa ajili ya kunywea katika eneo la biashara kwa watu waliopanga hotelini kwa wakati wowote wa mchana na usiku RESTAURANT Leseni hii inamruhusu mwenye leseni kuuza pombe kwa mtu yeyote anayekula chakula katika mgahawa katika muda wa saa 6.00 mchana hadi saa 8.00 mchana na saa 12.00 hadi saa 6.00 usiku. MEMBERS CLUB Leseni hii huruhusu uuzaji wa pombe kwa kiasi chochote kwa mwanachama wa Klabu na wageni wao tu COMBINED 4 Leseni ambazo zimeambatanishwa mhili kwa pamoja:
(a) Combined Hotel and retailers on
(b) Combined Hotel and Restaurant
(c) Combined restaurant and retailers on TEMPORARY Leseni hii humruhusu mwenye leseni kuuza pombe katika sehemu iliyotajwa kwenye leseni mahali penye burudani, starehe au mkusanyiko mwingine kwa kipindi kisichozidi siku tatu LOCAL LIQUOR Class A Local Liquor Leseni hii humruhusu mwenye leseni kutengeneza pombe za kienyeji katika sehemu iliyotajwa na kuuza kwa ajili ya kunywea sehemu ya biashara au nje ya sehemu ya biashara Class B Local Liquor Leseni hii humruhusu kutengeneza pombe ya kienyeji sehemu iliyotajwa na kwenda kuuzia sehemu nyingine iliyo na leseni ya kuuza pombe za kienyeji Class C Local Liquor Leseni hii humruhusu kutengeneza pombe ya kienyeji katika sehemu iliyotajwa kwenye leseni na kuuza kwa mwenye class D au Class E Class D Local Liquor Leseni hii humruhusu kuuza pombe za kienyeji katika sehemu iliyotajwa kwenye leseni kwa kunywea eneo la biashara Class E Local Liquor Leseni hii humruhusu kuuza pombe za kienyeji kwa ajili ya kunyewea sehemu nyingine mbali ya eneo la biashara
MASHARTI YA KUPATA LESENI
Mtu yeyote raia wa Tanzania anayo haki ya kupatiwa leseni ya Vileo ili mradi awe ametimiza umri wa miaka kumi na nane (18) mwenye akili timamu ambaye hajawahi kupatikana na kosa la jinai na awe na eneo la kufanyia biashara linalokubalika kisheria. Kwa mtu ambaye sio raia wa Tanzania anapaswa kuwa na kibali kinachomruhusu kufanya biashara nchini kutoka Idara ya Uhamiaji.
UTARATIBU WA KUPATA LESENI
• Mwombaji hujaza fomu za maombi zinazotolewa na Manispaa
• Eneo/jingo linalokusudiwa kufanyia biashara hiyo kukaguliwa na Afisa Afya, Afisa Mipangomiji, Polisi, Afisa Mtendaji wa Kata (WDC) na Afisa Biashara wa Manispaa na hutoa maoni yao kwenye fomu husika
• Maombi hayo hupelekwa katika Malaka ya Utoaji wa Leseni za Vileo ya Manispaa kwa uamuzi
• Mwombaji ambaye maombi yake yamepitishwa hupewa Leseni baada ya kulipa ada inayotakiwa na ni lazima amekamilisha masharti ya kupata leseni hapo juu MASHARTI YA UTUMIAJI Leseni za vileo zina masharti mengi ikiwa ni pamoja na kutouza kilevi 6 kwa watoto. Masharti mengine ni muda wa kuuza pombe na kelele za muziki. MUDA WA KUUZA POMBE BAA (RETAILERS ON) • Jumatatu hadi Ijumaa - Saa 12.00 jioni hadi saa 5.00 Usiku
• Jumamosi, Jumapili na Sikukuu - Saa 5.00 asubuhi hadi saa 8.00 mchana na saa 12.00 jioni hadi saa 6.00 usiku GROSARI (RETAILERS OFF)
• Jumatatu hadi Ijumaa - Saa 2.00 asubuhi hadi saa 1.00 jioni
• Jumamosi, Jumapili na Sikukuu - Saa 3.00 asubuhi hadi saa 6.00 mchana RESTAURANT LICENCE (MGAHAWA)
• Jumatatu hadi Ijumaa - Saa 6.00 mchana hadi saa 8.00 mchana na saa 12.00 jioni hasi saa 6.00 usiku
• Jumamosi, Jumapili na Sikukuu - Saa 5.00 asubuhi hadi saa 8.00 mchana na saa 12.00 jioni hadi saa 6.00 usiku MAKOSA Baadhi ya makosa chini ya sheria hii:
• Kuruhusu biashara nyingine isiyokubalika kisheria kufanyika eneo la biashara
• Kuuza pombe kwa mtu mwenye umri chini ya miaka kumi na sita (16)
• Kuajiri mtu chini ya miaka kumi na sita (16) kuuza pombe
• Kuruhusu mtu mwenye umri chini ya miaka kumi na sita kukaa eneo la kuuzia pombe
• Kutoweka leseni sehemu ya wazi, ambapo itaonekana kwa urahisi na wakaguzi
• Kumruhusu/kuleta fujo katika eneo la biashara
• Kuruhusu eneo la biashara kutumika kama danguro
• Kuuza pombe muda ambao ni kinyume cha sheria
• Kufanya biashara ya pombe kwa kutumia leseni ya vileo ambao haistahili ADHABU Mfanyabiashara anayetenda mojawapo ya makosa haya akikamatwa, atafikishwa mahakamani na akitiwa hatiani atalipa faini au kifungo au adhabu zote kwa pamoja.
UTARATIBU WA USHURU WA MALAZI (HOTEL LEVY) CHINI YA SHERIA NA. 23 YA 1972 MASHARTI YA KULIPIA HOTEL LEVY
1. Kila mmiliki wa nyumba ya wageni (Guest House) anapaswa kulipa kodi ya asilimia ishirini (20) ya malipo ya nyumba (Guest House charges) kwa mwezi husika. Wamiliki wenye mauzo yanayotozwa kodi ya zaidi ya Tshs. 40 milioni kwa mwaka hawatalipa kodi ya malazi bali watalipa Kodi ya ongezeko la tghamani (VAT)
2. Kodi iliyowekwa, italipwa kuanzia tarehe moja hadi tarehe saba ya mwezi unaofuata mauzo
UTARATIBU WA KULIPIA HOTEL LEVY
• Malipo ya Ushuru wa Malazi ni lazima yaambatanishwe na fomu ya mapato ya kila siku (fomu H.L. 1) au kitabu cha wageni, na fomu ya mapato ya kila mwezi (fomu H.L.2)
• Mmiliki wa nyumba analeta fomu H.L.1 au kitabu cha wageni pamoja na fomu H.L. 2 ambaye amekwisha jaza. Afisa anayekadiria atapitia H.L.1 au kitabu cha wageni na fomu H.L. 2 ili kuhakikisha ni sawa na kuhakikisha mmiliki amefikia vizuri asilimia 20 ya mapato ya malazi ya mwezi.
• Mmiliki akishindwa kulipa ushuru kwa muda uliopangwa, siku saba (7) baada ya mwezi husika kumalizika, atalipa nyongeza ya asilimia 25 ya ushuru unaotakiwa kulipwa, na endapo ataendelea kutokulipa adhabu (penalty) itakuwa inaongezeka kwa asilimia kumi (10) ya ushuru uliotakiwa kulipwa kila baada ya siku thelathini (30) kumalizika
MAKOSA
• Mmiliki wa nyumba ya kulala wageni kushindwa kulipa ushuru wa malazi kwa muda unaotakiwa
• Kushindwa au kukataa kuwasilisha fomu ya mapato ya kila mwezi
• Kushindwa kuweka na kutunza kitabu chenye kumbukumbu sahihi za kulala wageni
• Kushindwa kutoa risiti, hati za madai na kumbukumbu nyinginezo kama sheria inavyotaka
• Kumzuia Mkurugenzi au Mwakilishi wa Mkurugenzi katika kufanya kazi zake zilizowekwa na sheria au Kanuni za Ushuru wa Malazi
• Kushindwa kutekeleza Ilani iliyotolewa na Kamishna/mkurugenzi ya kuitwa na kuwasilisha nyaraka zinazohusu nyumba yake ya kulala wageni
• Kutoa taarifa ya uongo kwenye kumbukumbu yeyote inayotumika kwa ajili ya kudanganya au kushindwa au kukataa kujibu maswali vizuri kwa Afisa wa Serikali aliyepewa madaraka na sheria hii
ADHABU
• Mmiliki atakayetenda mojawapo ya makosa yaliyotajwa hapo juu atalipa faini isiyopungua Tshs. 50,000.00 kwa Mkruugenzi wa Manispaa na isiyozidi Laki tano (500,000.00) Mahakamani akipatikana na hatia.
• Mmiliki anayekwepa kulipa Ushuru wa Malazi kwa makusudi akikamatwa na kutiwa hatiani atalipa faini isiyozidi shilingi milioni mbili (2,000,000.00) Hata hivyo kila halmashauri ya wilaya na miji zina utaratibu wake ambao ni vema mfanyabiashara akachukua hatua katika kufahamu ili kuepuka uvunjaji wa kanuni za uendeshaji wa biashara na kuepuka adhabu.
NAWATAKIA MAADALIZI MEMA KATIKA KUFIKIA MALENGO YENU.
KUMBUKA "Usikate tamaa,lakini acha maneno anza vitendo"
Subscribe to:
Posts (Atom)