Wednesday, 25 January 2017
NMB YAIBUKA KIDEDEA
BENKI ya NMB imewekwa katika daraja la kwanza na kampuni ya kimataifa ya utafiti ya Moody’s Investors Service kwa uwezo wake wa kuhimili madeni na usalama wa kifedha.
Kampuni hiyo ya Moody’s ni moja ya kampuni zinazofanyia tathmini na kushindanisha utendaji wa taasisi za fedha duniani.
Kwa mujibu wa taarifa ya benki hiyo ya NMB kwa waandishi wa habari Dar es Salaam jana, daraja hilo linaifanya benki hiyo kuwa ni benki inayoongoza kwa kuwa na huduma bora na za uhakika katika nchi za Afrika isipokuwa Afrika Kusini.
“Benki hii imepata daraja hili baada ya kufanyiwa tathmini katika maeneo mbalimbali ikiwemo mazingira ya uendeshwaji wake, mazingira ya jumla pamoja na shughuli za kibiashara za benki hii,” ilisema taarifa hiyo ya benki.
Kupatikana kwa daraja hilo, kunaendana na malengo ya NMB ya kuhakikisha benki hiyo inakuwa ni taasisi ya fedha inayoongoza kwa kutoa huduma bora nchini.
Aidha, daraja hilo, linaonesha namna pia benki hiyo ilivyo imara na yenye akiba ya kutosha, lakini pia inayozingatia suala la utawala bora.
Bodi ya Wakurugenzi na menejimenti ya benki hiyo, imefurahishwa na kitendo cha benki hiyo kupatiwa daraja hilo, kwani kutaisaidia NMB kuwa katika nafasi ya kujadili masharti mazuri zaidi na watoa mikopo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment